Ruka hadi maudhui

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Majibu ya maswali kuhusu Ada ya Mwezi, kuhifadhi nyumba, malipo na mawakala.

Maswali tunayoulizwa

Bado una swali? Tupigie kwa +255 764 256 408 au tuandikie [email protected].

TSh 5,000 inalipia nini hasa?

Siku 30 za kupata mawasiliano ya mawakala kwenye kila tangazo ndani ya app. Unaweza kupiga simu, kutuma WhatsApp na kupanga kuona nyumba mara nyingi kadri unavyohitaji ndani ya mwezi huo.

Kuhifadhi nyumba kunafanyaje kazi?

Ukishachagua nyumba, unalipa ada ya kuhifadhi ya 30% ya kodi ya mwezi mmoja ndani ya app. Kisha unapewa mawasiliano ya mwenye nyumba na nyumba inaondolewa KodiSmart ili mtu mwingine asiichukue. Kodi unamlipa mwenye nyumba moja kwa moja.

Naweza kulipa kwa njia gani?

Mobile money: Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa. Utapokea ujumbe kwenye simu yako na kuthibitisha kwa PIN yako.

Itakuwaje nyumba isipofanana na maelezo?

Ripoti tangazo hilo kupitia app. Timu yetu italikagua pamoja na wakala na Meneja wake, na itawasiliana nawe kuhusu kurudishiwa pesa kama unastahili.

Mnahudumia maeneo gani?

Kwa sasa, Dar es Salaam peke yake: Kinondoni, Ubungo, Ilala, Temeke na Kigamboni. Miji mingine itafuata tukishapata mawakala huko.

Mawakala hulipwaje?

Mpangaji akihifadhi nyumba uliyoiorodhesha, unapata kamisheni. Timu yetu ya fedha hukagua kila kamisheni, na mapato yaliyoidhinishwa hutumwa kwenye namba yako ya mobile money tarehe 25 ya kila mwezi.

Nyumba yako ijayo huenda tayari iko hapa.

Bure kupakua. Bure kuangalia.

Inakuja hivi karibuniGoogle Play Mimi ni wakala